Paris Saint-Germain wamesitisha mkataba wa fowadi Jese Rodriguez miezi sita mapema kabla ya kufika mwisho.

Mchezaji huyo wa miaka 27 alijiunga na PSG kutoka Real Madrid mwaka 2016 lakini ametumia misimu minne kwa mkopo katika vilabu vinne tofauti.

Ameshiriki mara mbili kutoka benchi kwa mabingwa wa Ufaransa kwenye Ligue 1 msimu huu na alikuwa chini ya mkataba huko Parc des Princes hadi Juni 30, 2021.

Lakini, baada ya kuingiliwa na maswala kadhaa ya nje ya uwanja katika wiki za hivi karibuni, PSG wameamua kukatisha makubaliano na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uhispania ya chini ya miaka 21.

PSG ilithibitisha habari hiyo katika taarifa kwenye tovuti yao rasmi Jumapili na kuongeza: “Paris Saint-Germain inamtakia Jese kheri katika kipindi chote cha taaluma yake.”

Jese anaondoka mji mkuu wa Ufaransa akiwa amefunga mabao mawili katika mechi 18 kwenye mashindano yote.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Paris, Paris Saint-Germain Yavunja Mkataba na Jese., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

21 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa