Timu ya taifa ya Ghana imepata pigo kubwa kuelekea mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Dunia baada ya kiungo wake nyota, Thomas Partey, kunyimwa ruhusa ya kuingia nchini Canada. Shirikisho la Soka la Kimataifa limethibitisha kuwa ombi la viza la mchezaji huyo limekataliwa na mamlaka za Canada kutokana na kesi zinazomkabili nchini England.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Partey hataruhusiwa kusafiri kutoka kambi ya Ghana iliyopo Boston, Marekani, kuelekea Canada kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Panama unaotarajiwa kuchezwa Juni 17, 2026. “Shirikisho linaweza kuthibitisha kwamba mchezaji Thomas Partey hataweza kusafiri kutoka kambi ya timu ya Ghana iliyopo Boston, Marekani, kwenda Canada kwa ajili ya mechi yao ya kwanza dhidi ya Panama,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Taarifa hiyo imeeleza kuwa sababu ya kukataliwa kwa ombi la viza ni uamuzi wa mamlaka za Canada kufuatia kesi za ubakaji zinazomkabili mchezaji huyo nchini England. “Ombi lake la viza limekataliwa na serikali ya Canada,” iliongeza taarifa ya bila kutoa maelezo zaidi kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa baadaye.
Kutokuwepo kwa Partey kunatajwa kuwa pigo kwa Ghana, hasa kutokana na uzoefu wake mkubwa katika safu ya kiungo na mchango wake kwa timu ya taifa katika mashindano makubwa ya kimataifa. Benchi la ufundi sasa linalazimika kufanya mabadiliko ya haraka kabla ya mchezo huo muhimu dhidi ya Panama.
Wakati Ghana ikiendelea na maandalizi ya mwisho ya mechi hiyo, bado haijafahamika iwapo Partey ataweza kushiriki michezo mingine ya hatua ya makundi itakayochezwa nchini Marekani. “Kwa sasa mchezaji huyo atasalia kambini Boston hadi pale hatua zaidi zitakapobainishwa na mamlaka husika,” kilieleza chanzo cha karibu na timu hiyo.


