Patrick Vieira ametimuliwa na timu ya Ligue 1, Nice kufuatia kupoteza mechi tano katika msimu 2020-21.

Kocha huyo wa miaka 44 alikuwa akisimamia Nice tangu Juni 2018, kazi yake ya pili ya ukocha mkuu baada ya misimu miwili huko MLS na New York City FC.

Alitarajiwa kuwa nje ya mkataba mwishoni mwa kampeni lakini Nice wamechukua uamuzi wa kusitisha mkataba na nyota huyo wa zamani wa Arsenal.

Uamuzi huo umefanywa kufuatia kupoteza kwa 3-2 dhidi ya Bayer Leverkusen siku ya Alhamisi, ambayo iliambatana na maandamano ya mashabiki wakimtaka Vieira ajiuzulu.

Ushindi huo unahakikisha Nice haiwezi tena kusonga mbele kwa mtoano wa Ligi ya Uropa na wanashika nafasi ya 11 kwenye Ligue 1 baada ya kucheza mechi nyingi bila kuchukua alama.

Nice ilithibitisha habari hiyo kwenye tovuti yao rasmi siku ya Ijumaa na kutangaza Adrian Ursea ambaye alikuwa kocha msadizi kuchukua mikoba ya kuingoza Nice kwa muda.

“Katika mkutano uliofanywa baada ya mechi ya jana usiku, bodi ya Nice ilimjulisha Patrick Vieira juu ya uamuzi wao wa kusitisha wetu,” Nice ilisema katika taarifa.

“Rouge et Noir wameamua kumteua Adrian Ursea kama mkufunzi mkuu wa kikosi cha kwanza cha kilabu, kuanzia leo.”

Vieira aliongoza Nice hadi nafasi ya saba katika msimu wake wa kwanza kwenye msimamo wa Ligue 1 na akaiboresha kwa kumaliza nafasi ya tano katika msimu uliyokatishwa kufuatia kuwepo kwa janga la corona.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Patrick, Patrick Vieira Atimuliwa Nice., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

21 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa