Pedro Neto Aruhusiwa Kucheza Dhidi ya PSG Licha ya Tukio la Kumsukuma Ball Boy

Winga wa Chelsea, Pedro Neto, ameruhusiwa kucheza katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain baada ya refa  kumpa kadi ya njano kwa tukio la kumsukuma kijana wa kuokota mipira.

Pedro Neto Aruhusiwa Kucheza Dhidi ya PSG Licha ya Tukio la Kumsukuma Ball BoyTukio hilo lilitokea katika mchezo wa kwanza uliochezwa Parc des Princes, ambapo PSG waliibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Chelsea, matokeo yaliyoweka presha kubwa kwa timu ya England kuelekea mchezo wa marudiano.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kwa mujibu wa uchunguzi wa UEFA, Neto alipatikana na hatia ya utovu wa nidhamu uwanjani, na hivyo kuongezewa kadi ya njano kwenye rekodi yake, lakini hakuchukuliwa hatua kali zaidi inayoweza kumzuia kushiriki mchezo unaofuata.

Pedro Neto Aruhusiwa Kucheza Dhidi ya PSG Licha ya Tukio la Kumsukuma Ball BoyAkizungumza baada ya mchezo huo, Neto alikiri kosa lake na kueleza kuwa alichukuliwa na hisia za mchezo, akitaka kuharakisha urejeshwaji wa mpira wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao.

“Tulikuwa tunapoteza na katika presha ya mchezo nilitaka kupata mpira haraka, hivyo nikamsukuma kidogo. Mimi si mtu wa aina hiyo. Ilikuwa ni kutokana na hali ya mchezo na ninaomba radhi. Nilimpa jezi yangu na ninajutia sana kitendo hicho,” alisema Neto.

Pedro Neto Aruhusiwa Kucheza Dhidi ya PSG Licha ya Tukio la Kumsukuma Ball BoyNeto sasa anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea kitakachojaribu kupindua matokeo dhidi ya PSG, huku akiahidi kujifunza kutokana na tukio hilo na kuzingatia nidhamu ndani ya uwanja.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.