MSHAMBULIAJI mpya wa Simba Moses Phiri rasmi amekabidhiwa jezi namba 25 atakayokuwa anaitumia kwa msimu ujao huku mwenyewe akitamba kutaka kuweka rekodi mpya ndani ya timu hiyo.

Ukiachana na Phiri kukabidhiwa jezi hiyo pia imewahi kutumiwa na aiyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Emannuel Okwi ambaye alitamba na Simba akiwa na jzei namba 25.

Phiri alisema kuwa licha ya kukabidhiwa jezi hiyo ambayo tayari ameambiwa kuwa ni jezi yenye historia nzuri kwake imekuwa haimpi wasiwasi kwani ametamba kuweka historia yake mpya na yeye ndani ya timu hiyo.

“Nafahamu kila kitu kuhusu jezi namba 25,tayari nimeambiwa kuwa ina historia nzuri ndani ya timu hii,kwangu hii hainipi sana wasiwasi kwani na mimi nataka kuweka historia mpya nikiwa na hii jezi.

“Muhimu zaidi ni kuona Napata ushirikiano mzuri kutoka kwa familia nzima ambayo inanizunguka kwani naamini sitapata ugumu sana katika kuyazoea mazingira mapya,”alisema mshambuliaji huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa