Kipa wa England, Jordan Pickford, amesema kikosi chake kiko tayari kwa nusu fainali ya michuano ya Dunia dhidi ya Argentina na kimejipanga kuonyesha uwezo wake uwanjani badala ya kuingia kwenye malumbano. Pickford anaamini England imekuwa na nidhamu kubwa katika mashindano haya na itaendelea kuwa tulivu licha ya ukubwa wa mchezo huo.
Akizungumza katika kambi ya England iliyopo Kansas City, Pickford alisema timu yake imeonyesha ukomavu tangu mwanzo wa mashindano. “Katika mashindano yote mmeona namna tulivyojituma kushinda mipira bila kuingia kwenye ugomvi. Maamuzi yanaweza kwenda upande wetu au dhidi yetu, lakini tunajipanga upya na tunaiacha soka izungumze,” alisema kipa huyo wa Everton.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kuhusu Lionel Messi, ambaye anatarajiwa kuwa gumzo kubwa kabla ya mchezo huo, Pickford amesema England haitamwangalia yeye pekee bali itaamini ubora wa kikosi chake. “Watu wote watazungumza kuhusu Messi kwa sababu ni mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea, lakini pia hatupaswi kupuuza vipaji tulivyonavyo ndani ya kikosi chetu. Tunao uwezo mkubwa katika ushambuliaji, ulinzi na umoja wa timu,” alisisitiza.
Historia ya England na Argentina imekuwa na ushindani mkubwa kwa miongo kadhaa, ikiwemo mechi maarufu yamichuano ya Dunia 1986 iliyoshuhudia Diego Maradona akifunga bao la utata la ‘Mkono wa Mungu’ pamoja na bao lingine la kuvutia. Hata hivyo, Pickford amesema historia hiyo haina nafasi katika maandalizi ya sasa ya England.
“Ni sisi dhidi yao kwa nafasi ya kucheza fainali. Iwe dakika 90, muda wa nyongeza au mikwaju ya penalti, tuko tayari kwa kila kitu. Kilicho muhimu ni nani atakayemaliza akiwa mshindi,” alisema Pickford, akisisitiza kuwa England imejiandaa kikamilifu kwa pambano hilo muhimu.


