Gerard Pique anatumaini Barcelona watamshawishi Lionel Messi kuendelea kubaki katika klabu hiyo ya Spain kwa miaka mingi ijayo.

Messi, mwenye umri wa miaka 33 alionesha hisia zake kwa kuomba kuihama hiyo miamba ya LaLiga wakati wa kumaliza msimu uliyopita, lakini jaribio lake liligonga mwamba na kuendelea kusalia katika klabu hiyo.

Lakini, mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or mara sita amekuwa akihusishwa vilabu kama Manchester City, Paris Saint-Germain na Inter mara baada ya kumaliza kwa mkataba wake.

Lakini Pique anatumaini Messi atasalia Barcelona ambako ametumia maisha yake yote ya soka la kulipwa.

“Tutatakiwa kumuomba Messi. Ni maamuzi yake binafsi… na tutaona nini kitatokea,” beki huyo aliiambia Radio Marca siku ya Ijumaa.

“Nina amini kwa kuwa anaendelea kuvaa jezi ya Barca basi kuna tumaini.

“Tunaamini watamshawishi kwa hiyo atakaa kwa miaka mingi.

Messi amekuwa akipambana sana msimu kuwa katika fomu yake ya kawaida msimu huu, amefunga magoli sita peke katika mechi 11 magoli matatu ni kutoka kwenye michezo nane Laliga.

Messi hajafanikiwa kutengeneza asisti katika LaLiga wakati pia ana wastani 2.1 wa kutengeneza nafasi kwa dakika 90, rekodi duni tangu mwaka 2012-13.


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

16 MAONI

  1. Wachezaji mwezake messi wanamuhitaji ingawa viongozi mda mwingine wanajifanya hawamuhitaji kumbe wanatamani aendelee back

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa