Kocha wa Juventus,Andrea Pirlo amemsifu Christiano Ronaldo kwa kuuanza msimu mpya akiwa kwenye fomu na anatumaini ataendelea na kiwango hicho.

Ronaldo amefunga magoli 3 na kutoa asisti moja katika michezo miwili ya Serie A msimu huu 2020-21 na kuisadia Juventus kukusanya alama 4.

Pirlo: Ronaldo Atafunga Goli 1 au 2 Kila Mechi.
Kocha Andrea Pirlo na Christiano Ronaldo.

Kuelekea mchezo wa siku ya Jumapili dhidi ya Napoli, Kocha mkuu wa Juve Pirlo amemwagia sifa nyota huyo na kusema magoli mengi yanakuja kutoka kwa Ronaldo.

“Ronaldo anajituma sana, anakuwa wa kwanza kufika mazoezini na wa mwisho kurudi nyumbani,’ aliongea na waandishi wa habari.

“Naona ataendelea kufunga goli moja au mawili katika kila mchezo, ni mtu muhimu sana kwetu.

Ronaldo na Juventus wamepangwa watakabilaiana na Barcelona yenye Messi katika Champions League baada ya kupangwa kundi moja, wakati huo huo Dynamo Kiev na Ferencvaros pia wapo katika kundi hilo.

“Tupo kwenye kundi zuri, ni jambo zuri kuwakabili Barcelona kwa sababu inaleta jukumu la umakini kwa wachezaji wetu.” alisema.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

35 MAONI

  1. Ukiachana na ufungaji wa magoli katika clabu pia kuna hishindani na mpinzani wake messi ukiangalia sasa wachezaji chipukizi wana moto wa hajabu lazima hajitume hipasavyo ili kutunza ufalme wake

  2. Ukiachana na ufungaji wa magoli katika clabu pia kuna hishindani na mpinzani wake messi ukiangalia sasa wachezaji chipukizi wana moto wa hajabu lazima hajitume hipasavyo ili kutunza ufalme wake

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa