Kocha mkuu wa timu ya Juventus Andrea Pirlo amesisitiza Christiano Ronaldo hajapata umaalumu wowote katika klabu hiyo ya Serie A.

Ronaldo ameuanza msimu mpya vyema kwa kufanikiwa kufunga magoli nane katika michezo yake sita ya kwanza.

Aliweka kambani goli 2-0 mchezo ulipita siku ya Jumamosi dhidi ya Cagliari na Ronaldo alifikisha goli la 29 katika michezo 59 ya Juventus ndani ya Serie A.

Kuelekea mchezo wa Champions League siku ya Jumanne dhidi ya Ferencvaros, Pirlo alimuongelea Ronaldo na kusema mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or mara tano anachukuliwa kama wachezaji wengine.

“Nafanya naye kazi kama wachezaji wengine, mara nyingi napatikana uwanjani na nje ya uwanjani,” aliongea na waandishi.

“Ni rahisi kuwa na uhusiano mzuri na watu poa, nipo kama hivyo.

“nafanya naye kazi kama ninavyofanya na [Gianluca] Frabotta au [Manolo] Portanova ambao ni wachezaji makinda.

“Nafanya kitu hichohicho kama nilivyokuwa nafanya kipindi mimi ni mchezaji.

Magoli yote nane ya Ronaldo katika Serie A amefunga ndani ya box wakati pia ametengeneza nafasi kubwa nyingi.

Kuelekea kuwaongoza Ferencvaros, Juventus wapo nafasi ya pili katika kundi G alama tatu nyuma ya Barcelona.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

25 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa