INAELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Singida United,Hans Pluijm atatangazwa rasmi na benchi lake jipya Uwanja wa Liti Agosti 4 siku ya tamasha lililopewa jina la Big Day

Habari zinaeleza kuwa Singida Big Stars imefikia hatua nzuri na Pluijm kuweza kurejea kwa mara nyingine tena kwenye ardhi ya Tanzania aliwahi kuifundisha Yanga, Azam FC na Singida United.

Pluijm, Pluijm Kutambulishwa Agosti 4 Big Day, Meridianbet

Ofisa Habari wa Singida Big Stars,Hussein Masanza alisema kuwa kumekuwa na orodha ndefu kuhusu benchi la ufundi ila wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.

“Walianza kusema Zahera,(Mwinyi) na sasa ni Pluijim naona orodha inazidi kuwa ndefu hivyo ni suala la kusubiri na kuona kwani wakati unakuja.

“Agosti 4 tutatambulisha benchi la ufundi na orodha ya wachezaji wote wa kikosi kupitia event,(tukio) yetu ya Big Day mkoani Singida,” alisema Massanza.

Siku hiyo Singida Big Stars itatambulisha pia uzi mpya na itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Klabu ya Zanaco.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa