Kocha wa timu ya taifa ya Marekani, Mauricio Pochettino, amepongeza uamuzi wa FIFA wa kufuta adhabu ya kutocheza mechi moja kwa mshambuliaji Folarin Balogun, hatua inayomruhusu kuichezea Marekani dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya mashindano ya Dunia utakaopigwa Jumatatu mjini Seattle.
Balogun, ambaye tayari ameifungia Marekani mabao matatu katika mechi tatu za michuano hiyo, alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya mwamuzi kutumia VAR kwenye mchezo dhidi ya Bosnia na Herzegovina. Hata hivyo, Kamati ya Nidhamu ya FIFA ilitumia Kifungu cha 27 cha kanuni zake na kubadilisha adhabu hiyo kuwa kipindi cha majaribio cha mwaka mmoja, jambo lililozua mjadala mkubwa huku upande wa Ubelgiji ukieleza kushangazwa na uamuzi huo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Pochettino alisema timu yake ilikuwa tayari imeadhibiwa vya kutosha kwa kucheza zaidi ya dakika 30 ikiwa na wachezaji 10 dhidi ya Bosnia, hivyo aliona si haki kuendelea kumuadhibu Balogun kwa kukosa mchezo unaofuata.
“Ninaamini katika maadili na uadilifu wa mchezo huu, ndiyo maana tunasherehekea uamuzi huu. Tuliadhibiwa vya kutosha dhidi ya Bosnia kwa kucheza na watu 10 kwa zaidi ya dakika 30. Kadi ile ilikuwa si ya haki, hivyo hakukuwa na sababu ya kuendelea kumuadhibu Balogun,” alisema Pochettino.
Kocha huyo alifafanua kuwa hakuhusika moja kwa moja katika mchakato wa kukata rufaa, akisema shirikisho la soka la Marekani ndilo lililofanya kazi kubwa kuhakikisha adhabu hiyo inapitiwa upya. Pia alieleza kuwa kurejea kwa Balogun kunatoa matumaini makubwa kwa Marekani dhidi ya Ubelgiji, akisisitiza kuwa timu yake imeimarika tangu ilipopoteza kwa mabao 5-2 dhidi ya wapinzani hao katika mchezo wa kirafiki mwezi Machi.


