Kiungo wa Ufaransa Paul Pogba pamoja na Muitalia Federico Chiesa wamelazimika kutazama mwanzo mbaya wa Juventus msimu huu wakiwa nje ya uwanja lakini wanarajiwa kurejea kwa wakati na kumenyana na Benfica.

 

Pogba na Chiesa Kurejea Uwanjani Dhidi ya Benfica.

Bianconeri wamekuwa na mwanzo mbaya msimu huu chini ya Massimiliano Allegri, wakipoteza mechi zao mbili za kwanza za ligi ya Mabingwa na kusalia katika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa Serie A baada ya kupata ushindi mara mbili pekee katika mechi zao saba za kwanza za Serie A msimu huu.

Juventus wako katika hali ya majeruhi kidogo, wakiwa na wachezaji saba wa kikosi chao kukosekana, lakini mamabo yameanza kuwa sawa.

 

Pogba na Chiesa Kurejea Uwanjani Dhidi ya Benfica.

Kam ailivyoripotiwa na Ruttosport, Pogba na Chiesa wote wanafanya kazi kwa bidii ili kuwa fiti na wanatarajia kurejea katika kipindi cha mwezi mmoja, Juventus itamenyana na Benfica kwenye ligi ya Mabingwa mnamo Oktoba 25.

Kurejea kwao kungekipa kikosi cha Allegri nguvu kubwa na maisha baada ya kuanza kwa kusuasua, na klabu hiyo ina matumaini ya kuwasaidia kabla ya kombe la Dunia mwezi Novemba huko Qatar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa