Beki wa Hispania, Pedro Porro, amesema umoja wa kikosi na kazi ya kocha Luis de la Fuente ndiyo msingi wa mafanikio ya timu hiyo kuelekea nusu fainali ya michuano ya Dunia dhidi ya Ufaransa. Porro amesema Hispania imejijengea mazingira ya kifamilia yanayowapa nguvu ya kupambana katika kila mchezo.
Akizungumzia maandalizi ya pambano hilo, Porro alisema hana shaka na uwezo wa kikosi hicho licha ya safari nyingi walizofanya kwenye mashindano. “Hatuhisi uchovu. Tumeweza kurejea katika hali nzuri na sasa akili zetu zote ziko kwenye nusu fainali. Luis de la Fuente amekuwa mtu muhimu sana kwetu, ndiye aliyejenga umoja huu na kufanya kila mchezaji ajisikie sehemu ya timu,” alisema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Porro pia alieleza kuwa nafasi yake uwanjani hubadilika kulingana na aina ya mpinzani anayekutana naye. “Kila mechi ni tofauti. Wakati mwingine unalazimika kushambulia zaidi, wakati mwingine kujilinda. Dhidi ya Ubelgiji nilisaidia kushambulia, lakini pia nilikuwa na jukumu kubwa la kumdhibiti Doku. Kila kitu hutegemea mpinzani,” alifafanua.
Akikumbuka ushindi wa Hispania katika michuano ya Dunia la mwaka 2010, Porro alisema alikuwa mtoto mdogo sana lakini bado anakumbuka furaha ya kusherehekea ubingwa huo. “Nakumbuka nilikuwa naoga wakati Hispania ilipotwaa taji la Dunia, kisha tulienda Plaza de España kusherehekea. Leo kucheza nusu fainali ya michuano ya Dunia ni ndoto nyingine iliyotimia,” alisema.
Kuhusu mchezo dhidi ya Ufaransa, Porro amesema hakuna timu inayoweza kuitwa favorit katika hatua hiyo ya mashindano. “Hakuna anayepaswa kuitwa favorit katika hatua hii. Ni timu mbili kubwa na itakuwa mechi ngumu sana. Siri ya mafanikio yetu ni kubaki wamoja na kuucheza kila mchezo kana kwamba ni fainali,” alisema kwa kujiamini.


