Graham Potter amewasihi mashabiki wa Brighton kumsamehe kwa kuihama klabu hiyo na kuwa kocha mpya wa Chelsea.

Potter, (47), alitia saini mkataba wa miaka mitano Chelsea siku ya Alhamisi kumrithi Thomas Tuchel, ambaye alitimuliwa mapema wiki.

Potter:Naomba Mashabiki Wanisamehe

Katika barua ya wazi iliyoandikwa siku ya Alhamisi na kuchapishwa kwenye tovuti rasmi ya Brighton siku ya Jumapili, Potter alisema atafurahia ‘miaka mitatu akiwa na timu hiyo‘ huko Brighton lakini akakubali kwamba baadhi ya mashabiki hawataweza kumsamehe.

Graham alisema: “Hii imekuwa miaka mitatu ya ajabu na klabu ambayo imebadilisha maisha yangu na ninataka kuchukua muda kuwaaga ninyi nyote ambao mmefanya kipindi hiki maalum cha maisha yangu.

Potter:Naomba Mashabiki Wanisamehe

“Ninaaga klabu kubwa na ambayo daima itakuwa na maana sana kwangu na familia yangu. Kwa wengine natambua kuwa mabadiliko yanayokuja ghafla kwenye soka yanaweza kuwa magumu kuyakubali.”

 

“Huenda nisiweze kuwashawishi nyote kusamehe kuondoka kwangu, lakini ningependa angalau kuchukua nafasi ya kusema asante.” Graham alisema.

Kocha wa zamani wa Ostersunds na Swansea kocha huyo aliiongoza Brighton hadi nafasi ya tisa kwenye Ligi ya Uingereza msimu uliopita, umaliziaji wa juu zaidi katika ligi hiyo, na wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa sasa.

Potter:Naomba Mashabiki Wanisamehe

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa