Prince Dube amekua mtambo wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga SC ambacho kimefunga raundi ya 30 kwa ubao kusoma Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji, Juni 22 huku akiwa na hatihati kuukosa mchezo wa Kariakoo Dabi, Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa.
Prince Dube ambaye hakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa raundi ya 28 dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Juni 18 2025, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kwenye mchezo huo Dube alikomba dakika 22 nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama ambaye alifunga bao moja dakika ya 35 akitumia pasi ya Clement Mzize wakati ubao ukisoma Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Ndani ya ligi namba nne kwa ubora, Prince Dube kafunga mabao 13 akitengeneza pasi 8 za mabao ikiwa ni msimu wake wa kwanza kuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Prince Dube ni mchezaji wa kwanza kufunga hat trick msimu wa 2024/25 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Yanga SC imefunga jumla ya mabao 81 baada ya mechi 29 ikiwa ni timu namba moja kufunga mabao mengi. Dube kahusika kwenye mabao 21.