Kivumbi cha ligi kuu ya Ufaransa kinaendelea hii leo ambapo majira ya saa 21:45 usiku itawakutanisha mabingwa wa ligi hiyo Psg ambao watawakaribisha Monaco katika dimba lao la Parc Des Princes.

Psg kuwaalika Monaco.

 

Msimu iliopita timu hizi mbili waligawana alama sita huku kila mmoja akishinda nyumbani kwake bila ya kuruhusu nyavu zake kutikiswa. Toka league 1 iliporejea zimechezwa mechi nne kwa baadhi ya timu na tatu kwa timu zingine ambapo leo hii zote zitakamilisha mechi nne.

Psg yupo nafasi ya tatu na alama tisa katika michezo yote aliyocheza, huku akiwa  ameshinda mechi zote kwa ushindi mkubwa, na kwa upande wa Monaco yeye yupo nafasi ya 14 akiwa amecheza michezo mitatu  ameshinda mchezo mmoja na kupoteza mmoja.

psg, PSG Kuwaalika Monaco., Meridianbet

Mpaka sasa Psg ndiyo inaongoza kwa kufunga mabao mengi kwenye ligi hiyo ikiwa na jumla ya tofauti ya mabao 14, na mechi iliyopita walifunga mabao saba huku mshambuliaji wa timu hiyo Kylian Mbappe.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa