Paris Saint-Germain itamkosa Mauro Icardi na Pablo Sarabia kwa mechi kubwa ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano dhidi ya Manchester United.

PSG ambao walishika nafasi ya pili kwenye msimu uliopita wanalingana kwa alama na RB Leipzig na nyuma ya viongozi watatu United katika Kundi H.

Kikosi cha Thomas Tuchel hakina wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kwa mechi muhimu huko Old Trafford kwani Julian Draxler na Juan Bernat pia wanaonekana hawafai.

Icardi alirudi kutoka kuuguza marajeha baada ya kupunguzwa miezi miwili na ameumia tena goti katika sare ya 2-2 siku ya Jumamosi dhidi ya Bordeaux.

Lakini, PSG ilithibitisha kwenye tovuti yao rasmi kwamba mshambuliaji huyo alihisi maumivu kwenye mguu wake wa kulia wakati wa mazoezi na hatakuwa sehemu ya safari yao.

Mshambuliaji mwenzake Sarabia pia aliingia mwishoni kwenye mchezo dhidi ya Bordeaux lakini tangu acheze mchezo huo amepata jeraha la misuli.

Draxler na Bernat hawajacheza tangu Oktoba na Septemba wakati huo huo,wameondolewa rasmi kwenye kikosi kitakacho safiri kwenda Manchester.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Icardi, PSG Kuwakabili Man United Bila Sarabia na Icardi., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa