Timu ya QPR imeshindwa kuongoza ligi daraja la kwanza hapo jana baada ya  ilikosa nafasi ya kurejea kileleni kwenye msimamo baada ya kutandikwa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya Birmingham.

 

QPR Yashindwa Kurejea Kileleni Kwenye Msimamo.

Auston Trusty na Emmanuel Longelo ambao wametolewa kwa mkopo Arsenal na Westham, ndio walioiandikia Birmingham ushindi wa mabao katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Wakati dakika ya 79 ya mchezo, mlinda mlango wa Birmingham John Ruddy akiokoa mkwaju kutoka kwa  Lyndon Dykes na kuhakikisha kuwa wageni hawapandi katika nafasi ya kwanza. Hilo lilihitimisha kurejea vibaya West Midlands kwa kocha mkuu wa QPR Michael Beale, msaidizi wa zamani wa Steven Gerrard ambaye siku si nyingi ametimuliwa Aston Villa.

QPR Yashindwa Kurejea Kileleni Kwenye Msimamo.

QPR pia ilimpoteza mlinzi wa zamani wa Birmingham kwa mkopo Jake Clarke-Salter na mshambuliaji Tyler Roberts kutokana na majeraha kabla ya muda wa mapumziko. Bao la kizembe liliwapa Birmingham mwanzo mzuri wa kuongoza ndani ya dakika nne.

Lakini pia QPR hawakukata tamaa kwenye kufanya mashambulizi kwenye ango la wenyeji ambapo walipiga mashuti manne yaliyolenga lango, kona zilifika 10 na pia walikuwa na umiliki mkubwa wa mpira wa 60%.

QPR Yashindwa Kurejea Kileleni Kwenye Msimamo.

Baada ya kupoteza hapo jana sasa QPR wamebaki nafasi yao ile ile ya pili wakiwa na alama 30, huku vinara wa ligi hiyo ya daraja la kwanza wakiwa ni Burnley wakiwa na alama 32.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa