Kocha wa Ghana, Carlos Queiroz, amesema ukosefu wa mpangilio na nidhamu ya ulinzi ndiyo uliosababisha timu yake kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Colombia katika hatua ya 32 bora ya michuano ya Dunia 2026. Bao pekee la Jhon Arias katika dakika ya 14 liliiondoa Ghana kwenye mashindano na kuipa Colombia tiketi ya kucheza na Uswisi katika hatua ya 16 bora.
Queiroz alisema Ghana ilianza vizuri mchezo huo, lakini ilishindwa kucheza kwa kiwango kilichotarajiwa kutokana na makosa mengi ya pasi na kushindwa kujipanga vizuri baada ya mabadiliko ya mapema yaliyosababishwa na jeraha la beki wa kulia Marvin Senaya. “Ubora wa pasi zetu haukuwa kama tulivyotarajia. Tulifanya makosa mengi na tukaruhusu mashambulizi ya kushtukiza. Walifunga katika wakati ambao timu haikuwa imejipanga vizuri,” alisema Queiroz.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo alieleza kuwa jeraha la Senaya ndani ya dakika 10 za mwanzo liliathiri mpangilio wa timu, huku mbadala wake akiingia na Colombia kutumia mwanya huo kufunga bao la ushindi kupitia Arias. “Baada ya Senaya kutoka, timu haikuwa tena na nidhamu na mpangilio ule ule tuliokuwa nao mwanzoni mwa mchezo,” aliongeza.
Akizungumzia mustakabali wake, Queiroz ambaye aliteuliwa kwa mkataba wa muda mfupi uliokuwa na kipengele cha kuongezewa miaka miwili kulingana na matokeo ya michuano Dunia, hakutaka kuweka wazi hatua yake inayofuata.
“Kwa sasa ninachofuata ni kunywa glasi ya maji, kupumzika na kujituliza. Kesho ndipo nitaanza kufanya maamuzi mengine,” alisema Queiroz. Ghana sasa itarejea uwanjani mwezi Septemba kuanza kampeni za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 dhidi ya Ivory Coast.


