Kiungo wa Ufaransa, Adrien Rabiot, amesema kikosi cha Les Bleus hakiogopi Hispania wala hakijapanga mbinu maalum za kumzuia nyota wa Barcelona, Lamine Yamal, kuelekea nusu fainali ya michuano ya Dunia. Rabiot amesema maandalizi ya timu yake yamejikita katika kuikabili Hispania kama timu nzima badala ya kumlenga mchezaji mmoja.
Akizungumza kabla ya mchezo huo mkubwa, Rabiot alisema: “Hakuna mpango wa ‘anti-Yamal’. Tunaiangalia Hispania kwa ujumla wake, si mchezaji mmoja. Ni timu yenye hatari kila sehemu ya uwanja, hivyo tunapaswa kudhibiti mfumo wao wa uchezaji badala ya kumlenga mtu mmoja.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Rabiot pia alieleza kuwa kikosi cha Ufaransa kinaingia kwenye mechi hiyo kikiwa na imani kubwa baada ya safari nzuri iliyokuwa nayo kwenye mashindano. “Hatuogopi mtu yeyote. Kwa namna tulivyofika hapa, naamini tuko katika hali bora kabisa. Uwanja ndio utaamua matokeo, lakini sisi tumefanya kila linalowezekana kuwa tayari,“ alisema.
Kiungo huyo alibainisha kuwa siri ya mafanikio ya Ufaransa ni umoja uliopo ndani ya kikosi. “Tuna uhusiano mzuri sana nje ya uwanja na hilo limetupa nguvu kubwa. Pia tunajua hii ndiyo mashindano ya mwisho kwa kocha wetu akiwa na timu ya taifa, jambo ambalo linatupa motisha ya ziada kupigania ubingwa,” aliongeza.
Rabiot alisisitiza kuwa mawasiliano ya karibu kati ya wachezaji yamekuwa nguzo muhimu ya mafanikio yao. “Tunazungumza sana sisi kwa sisi, tunachambua mechi pamoja na kushirikiana mawazo. Wote tuna lengo moja na tunapambana kuelekea upande mmoja, jambo ambalo linaonekana wazi katika michezo yetu,” alisema.


