Rais wa CAF Afungiwa Miaka Mitano na FIFA.

Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad amefungiwa kwa kipindi cha miaka mitano na shirikisho la soka duniani FIFA kwa kukiuka sheria kadhaa za maadili.

Makamu huyo wa rais wa Fifa mwenye umri wa miaka 60 amedaiwa kukiuka sheria ya maadili inayohusisha jukumu lake la utiifu, kwa kutoa na kupokea zawadi hatua ambayo ni kinyume na nafasi yake mbali na matumizi mabaya ya fedha.

Rais wa CAF Afungiwa Miaka Mitano na FIFA.
Rais wa CAF, Ahmad Ahmad.

Uchunguzi kuhusu tabia ya Ahmad kutoka mwaka 2017 hadi 2019 ulihusu masuala ya utawala wake katika shirikisho hilo pamoja na kuandaa na kufadhili safari ya kuhiji Mecca, kuhusishwa kwake katika kashfa ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Tactical Steel na shughuli nyengine , ilisema taarifa ya Fifa.

Bwana Ahmad ambaye marufuku yake awali ilikuwa imetangazwa na BBCSport Africa , mwezi uliopita pia amepigwa faini ya $200,000.

Mwezi uliopita makamu huyo wa rais wa Fifa kutoka taifa la Madagascar alitangaza lengo lake kuwania muhula wa pili wakati uchaguzi wa Caf utakapofanyika mwezi Machi mwaka ujao.

Hilo huenda lisifanyike kwasababu atalazimika kupita mtihani wa maadili ili kustahiki kusalia katika baraza la Fifa.

Uwezekano wa yeye kuchaguliwa ka awamu ya pili utategemea iwapo atashinda kesi ya rufaa aliowasilisha katika mahakam ya kutatua mizozo ya michezo CAS , huku kesi hiyo akihakikisha kuwa inasikilizwa mapema ili kumruhusu kuthibitishwa kuwa mgombea.


Usichelewe Kukamata Mkwanja Huu!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

14 Komentara

    sheria lazima ifate mkondo wake kwa adhabu alio ipata itakuwa fundisho na kwa viongozi wengine wa soka

    Jibu

    Duuh hatar kubwa

    Jibu

    Majanga haya

    Jibu

    Duh

    Jibu

    Hii iwe fundisho kwa viongoz wengine wanaohujum soka

    Jibu

    Dhuu atalii

    Jibu

    Jamanii

    Jibu

    Sheria imefata mkondo wake

    Jibu

    Sheria ni msumeno inakata kata tu

    Jibu

    Shelia ni kazi

    Jibu

    Jmn

    Jibu

    Sheria aipingiki

    Jibu

    Duuh majanga ayo

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

Acha ujumbe