Klabu ya Rangers imemtimua kocha wao Giovanni Van Bronckhorst baada ya kushuka kwa kasi katika mbio za kuwania taji la ligi kuu ya Scotland.

 

Rangers Yamfukuza Kocha Wao

Van Bronckhorst alijiunga na Rangers Novemba mwaka jana kufuatia kuhamia kwa Steven Gerrard kwenda Aston Villa, na kuwaongoza kunyakua Kombe la Scotland na kufika fainali ya Ligi ya Europa ambapo walifungwa na Eintracht Frankfurt msimu uliopita.

Hata hivyo, kocha huyo hakujithibitisha kuonyesha kiwango chake kwani Rangers walimaliza msimu uliopita pointi nne nyuma ya Celtic na kuingia katika mapumziko ya Kombe la Dunia wakiwa nyuma ya pointi tisa dhidi ya wapinzani wao.

Rangers pia walivumilia kampeni ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, na kuwa timu ya kwanza ya Scotland kupoteza michezo yao yote sita ya hatua ya makundi kwenye shindano hilo, huku timu hiyo ikiruhusu mabao 22 katika mechi zote hizo, ambazo ni pamoja na kuchapwa 7-1 na Liverpool na kichapo cha 4-0 kutoka kwa Ajax.

Rangers Yamfukuza Kocha Wao

Katika taarifa yake kwenye tovuti ya Rangers siku ya Jumatatu, mwenyekiti Douglas Park alisema: “Nataka kumshukuru Gio kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miezi 12 iliyopita na, hasa mafanikio ya kuipeleka klabu hiyo fainali ya Ligi ya Europa na kushindwa.

Pia Mwenyekiti huyo alisema kuwa; “Kwa bahati mbaya matokeo ya hivi juzi hayajakidhi matarajio yetu wala ya Gio na tumechukua uamuzi huu mgumu leo. Kila mtu katika Rangers anamtakia Gio kila mafanikio katika siku zijazo”

Rangers Yamfukuza Kocha Wao

Huku kampeni ya Ligi Kuu ya Scotland ikiwa imesitishwa kwa Kombe la Dunia nchini Qatar, Rangers wana zaidi ya wiki tatu kutafuta mbadala wake kabla ya kuwakaribisha Hibernian mnamo Desemba 15.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Rangers, Rangers Yamfukuza Kocha Wao, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa