Raphinha anatarajiwa kuukosa mchezo wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Atletico Madrid baada ya kupata jeraha akiwa na timu ya taifa ya Brazi. Mchezaji huyo alipata maumivu wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa iliyochezwa nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Shirikisho la Soka la Brazil, Raphinha pamoja na beki wa AS Roma, Wesley, walipata maumivu kwenye misuli ya paja la kulia wakati wa mchezo huo. Vipimo vilivyofanyika siku iliyofuata vilithibitisha uwepo wa majeraha ya misuli kwa wachezaji hao wawili.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Klabu ya FC Barcelona imethibitisha kuwa mchezaji huyo atakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki tano huku akirejea Hispania kwa ajili ya matibabu maalum. Kukosekana kwake ni pigo kubwa kwa timu hiyo ya Catalonia, hasa ikizingatiwa mchango wake mkubwa msimu huu.
Raphinha, mwenye umri wa miaka 29, tayari amefunga mabao 19 msimu huu na atakosekana katika michezo yote miwili ya robo fainali dhidi ya timu ya kocha Diego Simeone. Barcelona itaanza kwa kucheza nyumbani Aprili 8 kabla ya kurudiana ugenini Aprili 14.
Mbali na michezo ya Ulaya, nyota huyo pia atakosa mechi muhimu za La Liga dhidi ya Atletico Madrid, RCD Espanyol, Celta Vigo na Getafe CF katika kipindi cha kupona kwake.
Barcelona ina matumaini kuwa Raphinha atakuwa fiti kurejea uwanjani kabla ya mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid Mei 10, au hata nusu fainali ya Champions League iwapo watafuzu. Aidha, anatarajiwa kuwa tayari kuichezea Brazil katika FIFA World Cup 2026 itakayoanza Juni 11.


