Klabu ya Real Betis imethibitisha kumsajili rasmi Antony kutoka Manchester United kwa ada ya awali ya pauni milioni 19. Hata hivyo, maelezo ya kina ya makubaliano hayo yameonyesha mabadiliko makubwa yanayoathiri namna United itakavyonufaika na uhamisho huo katika siku zijazo.
Awali, United walitarajia kupata asilimia 50 ya ada ya uhamisho wowote wa baadaye endapo Antony angeuzwa na Betis. Lakini kwa mkataba mpya, United sasa watapata asilimia 50 ya faida pekee ambayo Betis itapata iwapo itamuuza Antony. Hii inamaanisha kwamba iwapo Antony atauzwa kwa bei sawa na ile iliyolipwa sasa, United hawatapokea chochote, na watanufaika tu endapo thamani ya Antony itaongezeka zaidi ya gharama iliyolipwa.
Mkataba huo unaweza kufikia hadi pauni milioni 22.5 endapo vigezo vya nyongeza vitatimia. Malipo yamegawanywa kwa kipindi cha miaka mitano, na Real Betis italipa takribani pauni milioni 3.9 kwa mwaka, kiasi kinachokubaliana na bajeti ya klabu. Aidha, malipo yataongezeka kwa takribani pauni 435,000 kwa mwaka endapo Betis watafanikiwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya au kushinda taji lolote la Ulaya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa upande wa Manchester United, mabadiliko haya yana maana kuwa wamepunguza uhakika wa mapato ya baadaye na kubaki na faida ndogo pekee iwapo thamani ya mchezaji huyo itaongezeka. Hata hivyo, wamefanikiwa kumtoa mchezaji huyo kwenye orodha ya mishahara mikubwa, jambo linalopunguza mzigo wa kifedha klabuni.
Kwa Antony mwenye umri wa miaka 24, huu ni mwanzo mpya baada ya kipindi kigumu Old Trafford. Wakati akiwa na wakati mgumu kuonyesha kiwango chake cha Ajax, Real Betis wanamuona kama nyota mwenye kasi na ubunifu atakayewasaidia ndani ya La Liga na michuano ya Ulaya.