Real Madrid inatajwa kujiandaa kuwasilisha ofa ya pauni milioni 130 kwa Bayern Munich katika jitihada za kumsajili winga wa kimataifa wa Ufaransa, Michael Olise. Mabingwa hao wa Hispania wanaonekana kumuweka nyota huyo juu ya orodha yao ya usajili baada ya msimu wake bora akiwa Bundesliga.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za soka Ulaya, Rais wa Real Madrid, Florentino Pérez, anataka kumleta Olise kama moja ya zawadi zake za kwanza kwa kocha José Mourinho. “Perez anaamini Olise anaweza kuwa sehemu muhimu ya mradi mpya wa Real Madrid na kuongeza ubora katika safu ya ushambuliaji,” zimeeleza taarifa hizo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, Bayern Munich imeweka wazi msimamo wake kuhusu mchezaji huyo. Rais wa heshima wa klabu hiyo, Uli Hoeness, amesisitiza kuwa nyota huyo hayupo sokoni na kwamba viongozi wa Bayern hawana mpango wa kujadili uhamisho wake. “Olise ni sehemu ya mipango ya muda mrefu ya Bayern Munich na hatuko tayari kumpoteza,” inaelezwa kuwa ndiyo msimamo wa mabingwa hao wa Ujerumani.
Mbali na kukataa mawazo ya kumuacha aondoke, Bayern pia inaripotiwa kuandaa mpango wa kumuongezea mshahara ili kuimarisha uhusiano wake na klabu hiyo. Olise bado ana mkataba wa kuitumikia Bayern hadi mwaka 2029, hali inayowapa nguvu viongozi wa klabu hiyo katika mazungumzo yoyote yatakayojitokeza.



