Wachezaji wa timu ya taifa ya England, akiwemo Declan Rice, Marc Guéhi na Reece James, hawakufanya mazoezi pamoja na kikosi kizima Jumatano, badala yake walifuata programu maalum za mazoezi binafsi kuelekea mchezo wa robo fainali ya michuano ya dunia dhidi ya Norway.
Shirikisho la Soka la England lilithibitisha kuwa wachezaji hao watatu walipewa ratiba maalum ya maandalizi kutokana na hali zao tofauti za kimwili. England inatarajiwa kukutana na Norway Jumamosi katika mchezo utakaochezwa Miami, huku benchi la ufundi likiwa makini kuhakikisha wachezaji muhimu wanakuwa tayari kwa changamoto hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Reece James bado anafuatiliwa baada ya kukosa michezo mitatu katika mashindano haya kutokana na jeraha la misuli ya paja alilolipata kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Ghana uliomalizika kwa sare ya 0-0. Rice naye anaendelea kusimamiwa kutokana na tatizo la mishipa ya fahamu lililomsumbua mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu England akiwa na Arsenal FC.
“Rice amekuwa akisimamiwa kwa karibu kutokana na changamoto ya kiafya inayohusisha eneo la paja na mgongo wa chini. Alipumzishwa pia katika ushindi wa England wa mabao 2-0 dhidi ya Panama kwenye hatua ya makundi,” ilieleza taarifa ya timu hiyo.
England pia itamkosa beki Jarell Quansah katika mchezo dhidi ya Norway baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico katika hatua ya 16 bora iliyochezwa Estadio Azteca. Wakati huohuo, Rice, Guéhi, Harry Kane, Jude Bellingham na Nico O’Reilly wako kwenye hatari ya kukosa mchezo wa nusu fainali iwapo watapata kadi nyingine ya njano dhidi ya Norway.


