Nyota wa Al Nassr FC, Cristiano Ronaldo, ameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Saudi Pro League baada ya kuonyesha kiwango bora katika msimu huu.
Ronaldo ameendelea kuwa mhimili mkubwa wa mafanikio ya Al Nassr baada ya kufunga mabao 26 na kutoa pasi mbili za mabao, takwimu ambazo zimemuweka miongoni mwa wachezaji bora wa ligi hiyo msimu huu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Portugal ameisaidia Al Nassr kuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Saudi Pro League, huku timu hiyo ikihitaji alama tatu pekee kuthibitisha ubingwa wa msimu huu.
Uwezo wa Ronaldo ndani ya uwanja umeendelea kuwavutia mashabiki wengi wa soka duniani licha ya umri wake, huku akionyesha ubora mkubwa wa kufunga na kuiongoza timu yake katika mechi muhimu za msimu.
“Cristiano Ronaldo ameendelea kuthibitisha ubora wake kwa kuwa mmoja wa wachezaji wenye mchango mkubwa katika Saudi Pro League msimu huu,” zimeeleza taarifa kutoka ndani ya ligi hiyo.


