Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo, amesema ni “bahati ya maisha” kwamba ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Croatia katika hatua ya mtoano ya michuanoo ya Dunia umefanyika karibu mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa mchezaji mwenzake, Diogo Jota. Baada ya mchezo huo, Ronaldo na wenzake waliinua jezi namba 21 ya Jota kama ishara ya heshima kwa marehemu.
Ronaldo amesema kikosi kizima kilizungumzia kumbukumbu hiyo kabla ya mchezo na kwamba ushindi huo ulikuwa na maana ya kipekee kwao. Nyota huyo pia alivaa jezi yenye namba 21 wakati wa mahojiano baada ya mechi ili kuendelea kutoa heshima kwa Jota.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Ni bahati ya maisha, jambo la kushangaza sana. Tulilijua kabla ya mchezo na tulizungumza kuhusu kumbukumbu hiyo. Ilikuwa wakati wa kipekee kwetu sote,” amesema Cristiano Ronaldo.
Kocha wa Ureno, Roberto Martínez, amesema ushindi huo umeleta furaha kubwa kwa taifa la Ureno na pia umebeba ujumbe wa kumuenzi Diogo Jota. Amesema kufuzu hatua inayofuata katika mwaka wa kumbukumbu ya mchezaji huyo ni jambo lenye hisia kubwa kwa timu na mashabiki.
“Huu ni siku ya furaha kwa mashabiki wa Ureno. Tumefuzu hatua inayofuata, lakini pia tumemuenzi Diogo Jota katika mwaka wa kumbukumbu yake,” amesema Roberto Martínez. Diogo Jota na ndugu yake André Silva walifariki dunia Julai 3 mwaka jana baada ya kupata ajali ya gari nchini Hispania walipokuwa wakielekea kurejea England kujiunga na maandalizi ya msimu mpya.


