Mshambulliaji myota wa klabu ya Manchester United Ronaldo amesafiri na familia yake kwenye Private Jet yenye thamani ya £20million kwenda kwenye visiwa vya Majorca ambavyo viko nchini Hispania.
Baada ya UEFA nations League kusimama, sasa ni muda wa mapumziko ambapo wachezaji wengi nchini ulaya wamesafiri kwenda sehemu mbalimbali kwa ajiri ya kupumzika na kufarahia na familia zao, ambapo Ronaldo ametengeneza vichwa vya habari kwa kusafirisha magari yake ya thamani kwenda nayo mapumzikoni.
Cristiano Ronaldo amesafirisha gari yake yenye thamani ya £8.5milioni aina ya Bugatti Centodieci, ambayo ni miongoni mwa gari chache ambazo hutengenezwa kwa order maalum, pamoja na Mercedes SUV kwa ajiri ya familia yake ambazo zote zimeshafika kwenye visiwa vya Majorca.
Ronaldo amefikia kwenye hotel ambayo gharama zake kwa usiku mmoja ni £10,000, ndani yake kuna private villa, uwanja wa mpira, Gym binafsi, uwanja wa volleyball na Jacuzzi kadhaa,huku akiwa na familia yake ya watoto watano na mpenzi wake wa muda mrefu Georgina Rodriguez
Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wawili wenye mikataba ya maisha na kampuni ya Nike, huku pia akiwa na mkataba maalum na kampuni ya magari ya Bugatti.
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.