Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo alishaomba kuondoka kwenye klabu hiyo licha ya uongozi kutoonesha nia ya kutaka kumuachia msimu lakini amesisitiza kuondoka kabla ya dirisha la usajiri kufungwa.

Mpaka sasa CR7 ameendelea kuchukua vichwa habari kwenye magezeti mengi barani ulaya na kwenye mitandao ya kijamii kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka nchini ureno kuhusu uwelekeo wake, baada ya kuachana na mashetani wekundu.

Ronaldo

Mmiliki mpya wa klabu ya Chelsea ni mmoja ya watu wanaovutiwa na CR7 na yuko tayari kumvuta darajani kabla ya dirisha la usajiri kufungwa, ikiwa atakubali kubaki nchini Uingereza.

Ukiondoa klabu ya Chelsea vilabu vingine ambavyo wanahitaji huduma ya Cristiano Ronaldo ni Paris Saint-Germain na Bayern Munich ambapo awali walikana kuwa hawamuhitaji mshambuliaji huyo kwa sasa.

Moja ya sababu kubwa ambayo inamuondoa Ronaldo kwenye klabu ya Manchester United ni kuktokushiriki ligi ya mabingwa ulaya.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa