Cristiano Ronaldo ameteuliwa katika timu ya Wanaume ya Mwaka ya UEFA kwa mwaka wa 17 mfululizo lakini haishangazi ni washindi wa Ligi ya Mabingwa Bayern Munich ambao wanatawala.

UEFA ilitangaza orodha yake fupi ya majina yanayo wania kuingia kwenye timu ya UEFA ya mwaka kura zitakazo pigwa na mashabiki na Bayern iliongoza kwa kuwa na wachezaji wengi, wachezaji 10 – pamoja na usajili mpya wa Liverpool Thiago Alcantara akijumuishwa.

Ronaldo Kwenye Kinyang'anyiro cha Timu ya Mwaka ya UEFA.
Wachezaji Wateule wanao wania Timu ya mwaka ya UEFA 2020.

Bayern imetwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya sita mwezi Agosti, ikiifunga Paris Saint-Germain bao 1-0 kwenye Uwanja wa Estadio da Luz huko Lisbon.

Kingsley Coman, mfungaji wa bao la ushindi katika fainali, ni miongoni mwa wachezaji wa Bayern walioteuliwa, wakati Robert Lewandowski – mfungaji bora na 15 wa muhula uliopita anaonekana kuwa na nafasi kubwa katika XI.

Ronaldo yupo tena, mwaka wa 17 mfululizo ambapo ameteuliwa, kwani anatarajia kuongeza rekodi yake ya kuingizwa kwa 14 kwenye safu hiyo. Anamwacha mara nne Lionel Messi, ambaye pia anawania tena.

Alphonso Davies, 20, ndiye mchezji kinda zaidi wakati mkubwa ni Thiago Silva, mwenye umri wa miaka 36, ​​ambaye aliisaidia PSG kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kujiunga na Chelsea msimu huu.

Ligi ya premia na Bundesliga ni ligi zinazowakilishwa zaidi na wachezaji 15

UEFA pia iliweka orodha fupi ya Timu ya Wanawake ya Mwaka, na washindi wa Ligi ya Mabingwa ya Wanawake Lyon wakiwa na wachezaji wengi zaidi 13 – ikimuhusisha Lucy Bronze aliyeondoka tangu zamani katika ligue 1.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Ronaldo, Ronaldo Kwenye Kinyang’anyiro cha Timu ya Mwaka ya UEFA., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa