Ruben Dias kuondoka Manchester City baada ya Guardiola kuondoka

Beki wa kati wa klabu ya Manchester City, Ruben Dias, ameripotiwa kumuagiza wakala wake kuanza kutafuta uwezekano wa uhamisho wa kuondoka ndani ya dirisha hili la majira ya joto kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola.

Ruben Dias kuondoka Manchester City baada ya Guardiola kuondokaTaarifa kutoka karibu na klabu hiyo zinaeleza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 hajaridhishwa na mabadiliko ya kiufundi yanayoendelea ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa zamani wa England. “Ruben anafikiria mustakabali wake kwa umakini mkubwa baada ya mabadiliko yaliyotokea ndani ya klabu,” kilieleza chanzo cha karibu na beki huyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Dias alijiunga na Manchester City mwaka 2020 akitokea Benfica na tangu wakati huo ameichezea timu hiyo jumla ya mechi 255 katika mashindano yote. Uwepo wake ulikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya City chini ya Guardiola, ambapo alisaidia klabu hiyo kutwaa mataji mbalimbali ya ndani na kimataifa.

Ruben Dias kuondoka Manchester City baada ya Guardiola kuondokaLicha ya kuwa bado ana mkataba unaotarajiwa kumalizika mwaka 2029, ripoti zinaeleza kuwa klabu kadhaa kubwa barani Ulaya zimeanza kufuatilia hali yake kwa karibu. Real Madrid, Bayern Munich pamoja na Paris Saint-Germain zinatajwa kuwa miongoni mwa timu zinazohitaji huduma za beki huyo.

Ruben Dias kuondoka Manchester City baada ya Guardiola kuondoka“Dias bado ana thamani kubwa sokoni kutokana na uzoefu na ubora wake,” kiliongeza chanzo hicho huku thamani yake ikikadiriwa kufikia euro milioni 60. Hatma ya beki huyo sasa inasubiriwa kwa hamu huku mashabiki wa Manchester City wakihofia kumpoteza mmoja wa viongozi muhimu wa safu ya ulinzi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.