Mchezaji wa klabu ya Real Madrid Antonio Rudiger amemsifu kocha wa klabu hiyo Carlo Anchelotti na kusema hajawahi kufundishwa na kocha kama muitaliano huyo.

Rudiger anasimulia mkasa uliomfanya kumuona Carlo ni kocha wa kipekee tofauti na ambao amewahi kukutana nao hapo kabla.

rudiger“Tulikua kwenye nyumba yetu mpya na familia yangu kwa muda fulani, mpaka kengele ya mlango ilipolia. “Nilipoenda kufungua nakutana na Carlo amesimama mbele yangu,Tulikaa mezani pamoja tukala pamoja pia na kuijua familia yangu na alikua kawaida kabisa”.

“Alikaa na sisi kwa muda wa masaa mawili, Tuliongea kila kitu”.”Niseme ukweli sijawahi kukutana na kitu kama hicho mwalimu yeyote kufanya kama jivi kwangu”. Baada ya miezi michache ya kuishi naye naweza kusema Carlo kwenye suala la kuishi vizuri nawachezaji hana mfano”.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza amejaribu kuelezea ulimwengu ni namna gani kocha wa klabu hiyo amekua na uwezo wa kuishi na wachezaji wake vizuri na kuweza kupata kila kilicho bora kwa wachezaji hao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa