Bondia Ryan Garcia alipigana vyema dhidi ya mpinzani bora zaidi siku ya Jumamosi kwa kumpiga kwa KO Javier Fortuna katika raundi ya sita kwenye pambano la pauni 140 mjini Los Angeles.

Ryan Garcia Aendeleza Rekodi ya Kutopigwa

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 alimlambisha mchanga Fortuna katika raundi ya 4, 5 na ya sita akamaliza shughuli na konde la kushoto na Fortuna alipohesabiwa na mwamuzi alishindwa kuonyesha ishara ya kwamba anaweza kuendelea na pambano.

Sasa ameendeleza rekodi yake ya kutopoteza kwenye mapambano 23 aliyocheza na ameshinda KO kwenye mapambano 19  anatizamia kuchapana na Gervonta Davis pambano lijalo kama ikitokea.

“Ninajua kwamba nilikuwa mkali. … najua jinsi nilivyo mpiganaji mzuri, ilinibidi tu kuyaweka pamoja,” Garcia (23-0, 19 KO) alisema. “Pambano linajieleza lenyewe. … Ninapokabiliana na wapigaji ngumi kali zaidi, mimi hupiga ngumi vizuri zaidi. … napiga kwa nguvu; haichukui muda mwingi kumuumiza mtu.”


CHEZA KASINO HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa