Saibari Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Eredivisie, Godts Aibuka Kipaji Bora

Kiungo wa PSV Eindhoven, Ismael Saibari, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie) baada ya kuwa nyota muhimu katika mafanikio ya PSV kutwaa ubingwa kwa tofauti ya pointi 19 msimu huu.

Saibari Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Eredivisie, Godts Aibuka Kipaji BoraSaibari mwenye umri wa miaka 25 alifunga mabao 15 na kutoa pasi nane za mabao katika michezo 27 aliyocheza. Nyota huyo wa kimataifa wa Morocco aling’ara zaidi mwezi Oktoba wakati PSV ilipoifunga Feyenoord, ambapo alifunga hat-trick iliyowapeleka kileleni mwa msimamo kabla ya kutwaa ubingwa huo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya kushinda tuzo hiyo, Saibari alisema mafanikio hayo ni jambo kubwa kwake baada ya kutwaa mataji matatu ya ligi akiwa na PSV. “Baada ya kushinda ligi mara tatu, hii ni kama kilele cha mafanikio yangu,” alisema Saibari.

Saibari Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Eredivisie, Godts Aibuka Kipaji BoraSaibari aliwashinda wachezaji wengine waliowania tuzo hiyo akiwemo Joey Veerman, Mika Godts, Tjaronn Chery na Jacob Trenskow. Tuzo hiyo hupigiwa kura na manahodha wa timu zote 18 za Eredivisie.

Saibari Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Eredivisie, Godts Aibuka Kipaji BoraWakati huo huo, nyota wa Ajax, Mika Godts, ametwaa tuzo ya Johan Cruyff Talent of the Year baada ya msimu bora aliocheza kwa kufunga mabao 17 na kutoa pasi 12 za mabao. Godts alimshukuru mshambuliaji wa zamani Klaas-Jan Huntelaar kwa kumuamini tangu ajiunge na Ajax.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.