Alichokisema Saleh Jembe, Urejeo wa MO Dewji Simba

MCHAMBUZI na Mwandihi nguli wa habari za michezo Saleh Jembe, ametoa mtizamo wake juu ya kile kinachoendelea kwenye klabu ya Simba, ambapo MO Dewji ametangaza rasmi kurudi kwenye nafasi yake ya zamani kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba. Meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtanndaoni na sloti, cheza sasa ushinde Mamilioni

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram aleh Jembe alichapish ujumbe huu;

“Ukimsikiliza Salim Try Again wakati akitangaza kuachia NGAZI na baadaye ukamsikiliza Mohammed Dewji ambaye amerejea kwenye kiti cha Mwenyekiti wa Bodi alichokishika kwa mafanikio makubwa utagundua kuwa SIMBA INAREJEA KWENYE UHAI…

“Viongozi hao wawili wamekiri kuwa walikutana na kuzungumza na kauli aliyeachia NGAZI na anayetarajia kurejea WAMELENGA KUIREJESHA Simba iliyoirudisha heshima ya Tanzania katika michuano ya Caf.

“Kauli zote zimelenga kurejesha umoja na UBORA wa klabu ya Simba ambao UMEPOROMOKA… Kauli zao zimeonyesha ukomavu na tofauti kubwa na viongozi tuliowasikia siku CHACHE zilizopita, hawa wameonyesha maslahi ya klabu kwanza.

“Mambo muhimu mawili yataisaidia Simba kwa kuwa Kauli pekee hazitoshi…Moja kauli ZIWE THABITI….Pili NIA IWE SAHIHI na baada ya hapo Wanasimba Waungane. Mafanikio ya Simba kimataifa mfululizo yameleta MABADILIKO MAKUBWA kwa timu nyingine za Tanzania na heshima kubwa kwa taifa letu.”

“Ichukulieni Simba kama tunu ya taifa hili inayopaswa kutunzwa, kujaliwa na kusimamiwa kwa umakini na NIA THABITI. Kuachia NGAZI kutampa heshima Try Again kama kiongozi aliyejitambua na kuikubali hali halisi….”

“Uongozi ni dhamana …huwezi kudumu nayo milele na huu ni mfano wa uongozi Bora…Sasa muhimu Simba IKALENGA kwenye kujijenga UPYA…. mengine YAMEPITA …Safari ya maisha lazima kuna MILIMA na MABONDE..,”

Acha ujumbe