Mshambuliaji wa Aston Villa, Mtanzania Mbwana Samatta jana aliifungia timu yake bao pekee katika sare ya 1-1 waliyoipata katika Mchezo wa kirafiki dhidi ya Bristol City inayojiandaa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini England EFL Championship 2020/21.

Mchezo huo ambao Aston Villa wameutumia kama sehemu ya maandalizi ya kuelekea kuanza kwa msimu wa EPL 2020/21 ulichezwa kwa dakika 120 (60 kipindi cha kwanza na 60 kipindi cha pili) bila uwepo wa mashabiki.Bao la Bristol lilifungwa na Jamie Paterson.

Samatta, Samatta Anatesti Mitambo, Aweka Moja Kambani., Meridianbet

Samatta mwenye umri wa miaka 27 alisajiliwa na klabu ya Aston Villa mwezi Januari akitokea klabu ya Genk amefunga goli 1 katika Premier League kwenye michezo 14 aliyocheza, pia kulikuwa na tetesi kwamba Villa wanampango wa kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo kwenda klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki.

Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Villa tangu walipo kwenda sare na West Ham United mwezi Julai.

Kikosi cha kwanza kimekuwa kikijiandaa kambini na msimu mpya wa Primier League zaidi ya wiki moja sasa na Dean Holden amecheza mchezo wa kwanza kujipima kabla msimu haujaanza.


 

Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

42 MAONI

  1. Mbwana samatta ni mchezaji mzuri sana kama watampa nafasi zaidi mana tunaona katika michezo ambayo ana cheza huwa unakuwa kama ya ubaguzi sana kupata nafasi ya kuwa na mpira katika kujituma kwake kama ingekuwa wachezaji wanashirikiana vya kutosha nafikiri angekuwa mtanzania wa kwanza mwenye uwezo wa juu wa kufunga magoli mengi katika timu yake ya Aston villa pongezi sana samatta

  2. Wakati Aston Villa ina mnunua alitarajiwa kuleta mchango mkubwa na kuinusuru timu isishuke daraja. Ni kweli timu haijashuka daraja kwa kubahatisha mno#meridianbettz

  3. Samata hana jua sana mpila ila kuna ubaguzi kidogo unafanyika pale aston villa yani kama wanampa nafasi naimani kuna mengi mazuri kutoka kwake watayapata

  4. samatta yupo vizuri sana katika mpira na anajituma sana nina imani katika msimu ujao akipewa ushirikiano wa kutosha ataweza uonesha maajabu yake zaidi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa