Winga wa zamani wa Manchester United, Jadon Sancho, ameonekana akifanya mazoezi na klabu ya Flixton inayoshiriki Ligi ya Daraja la 10 nchini England, huku akiendelea kujiweka fiti baada ya kuwa mchezaji huru kufuatia kuachwa na Manchester United.
Sancho mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Manchester United mwaka 2021 akitokea Borussia Dortmund kwa ada iliyokadiriwa kufikia pauni milioni 73, lakini alishindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa ndani ya dimba la Old Trafford. Baadaye aliondolewa kwenye kikosi cha kwanza baada ya kudai hadharani kuwa alifanywa “mbuzi wa kafara.”
mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu
Baada ya kuondoka Manchester United, Sancho alirejea Borussia Dortmund kwa mkopo kabla ya kucheza msimu mmoja Chelsea, ambapo alifunga bao katika fainali ya UEFA Conference League. Msimu wa 2025/26 alitolewa kwa mkopo Aston Villa na alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa taji la Europa League, ingawa hakupata nafasi ya kudumu kikosini.
Aston Villa haikuchukua hatua ya kumsajili moja kwa moja baada ya mkopo kumalizika, hivyo Sancho alirejea Manchester United kabla ya kuachwa rasmi mwezi Juni. Kwa sasa, klabu ya Al Rayyan ya Qatar inatajwa kuwa miongoni mwa zinazowania saini yake.
Akizungumza baada ya kufanya mazoezi na Flixton, Sancho alisema: “Ninaishukuru Flixton kwa kunipa nafasi ya kufanya mazoezi hapa. Mazingira na vifaa vya klabu ni bora, na vinaendelea kunisaidia kujiandaa kwa hatua inayofuata katika maisha yangu ya soka.”


