Jadon Sancho amekuwa hayupo kwenye fomu nzuri msimu huu lakini atarejea kwenye kiwango chake bora katika timu ya Borussia Dortmund, hii ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo Michael Zorc.

Baada ya kuwa na msimu mzuri wa 2019-20 ambapo alifunga mabao 20 na kutoa asisti 19 katika michezo 44, Sancho anapambana kuwa kwenye fomu msimu huu.

Sancho Atarejea Kwenye Ubora Wake - Zorc.
Kiungo wa Dortmund, Jadon Sancho.

Katika michezo 12, mchezaji huyo wa kimataifa wa England ametikisa nyavu mara tatu na kutoa asisti nne, na bado hajaanza kufunga katika Bundesliga.

Akizungumza kabla ya safari ya Dortmund kwenda Eintracht Frankfurt Jumamosi, Zorc alimuunga mkono mshambuliaji huyo.

“Ninaamini ni rahisi kuona kwamba hayuko katika kiwango bora,” aliambia mkutano wa waandishi wa habari.

“Ninaweza kusema anajaribu kwa bidii wakati anaingia kwenye uwanja. Anajaribu kulazimisha wepesi na maji ambayo amejiweka mwenyewe.

“Jadon ni mchezaji ambaye hasemi mengi lakini anayetoa majibu uwanjani. huenda ikawa ni kesho au wiki ijayo au wakati mwingine, sijui.

“Ninachojua ni kwamba itatokea.”

Akiwa bado anahusishwa na kuhamia Manchester United, Sancho anapewa nafasi chache huko Dortmund.

Nafasi yake kubwa kwa dakika 90 katika Bundesliga msimu huu ni wastani wa 0.33 – ya chini kabisa tangu aanze kucheza kwenye ligi ya Ujerumani mwaka 2017.

Lakini, Sancho amepiga mashuti zaidi (2.15 kwa dakika 90) na mashuti kutoka ndani ya boksi (1.49) kuliko msimu mwingine wowote.

Huku Erling Haaland akiwa nje kwa sababu ya jeraha la nyama ya paja, Dortmund – ambao ni wa nne kwenye jedwali la Bundesliga – watakuwa na matumaini kuwa Sancho anaweza kurudisha fomu yake ya kufunga kumaliza 2020.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Sancho, Sancho Atarejea Kwenye Ubora Wake – Zorc., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

23 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa