Aliyekuwa kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Hispania, Santi Cazorla, ametangaza rasmi kustaafu soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 41. Cazorla anamaliza safari yake ya miaka 23 akiwa amecheza mechi 776 katika vilabu sita tofauti, zikiwemo nyakati tatu akiwa Villarreal na misimu sita yenye mafanikio akiwa Arsenal.
Katika kipindi chake Arsenal, Cazorla alisaidia klabu hiyo kutwaa mataji mawili ya Kombe la FA, huku akiwa pia sehemu ya kikosi cha Hispania kilichotwaa ubingwa wa Euro 2008 na Euro 2012. Alirejea katika klabu yake ya utotoni, Real Oviedo, mwaka 2023 na kuchangia kwa kiasi kikubwa kupandisha timu hiyo hadi LaLiga mwishoni mwa msimu wa 2024/25.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Leo ndiyo mwisho wa safari yangu kama mchezaji wa Real Oviedo, lakini si mwisho wa uhusiano wangu na klabu hii. Baada ya maisha yote niliyoyatoa kwa soka, sasa ni wakati wa kupumzika na kufikiria hatua inayofuata,” amesema Cazorla kupitia mitandao yake ya kijamii.
Baada ya Real Oviedo kushuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita, Cazorla aliamua kutoongeza mkataba wake na sasa anatarajiwa kuanza maisha mapya ya ukocha. Klabu hiyo imeeleza kuwa milango yake itaendelea kuwa wazi kwa nyota huyo kwa nafasi yoyote atakayochagua siku zijazo.
“Santi anajua kuwa milango ya Real Oviedo itakuwa wazi kwake kila wakati. Hapa ni nyumbani kwake, na tunatumaini kuendelea kushirikiana naye katika jukumu lolote litakalomletea furaha,” imesema Real Oviedo katika taarifa yake.


