Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Bukayo Saka amesema kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kumewanyamazisha waliokuwa wakiibeza klabu hiyo kwa miaka mingi, baada ya Arsenal kumaliza ukame wa miaka 22 bila taji hilo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tulikuwa kwenye kipindi kigumu sana, watu walikuwa wanatutania na kutucheka kila mahali, lakini sasa yote yamekwisha. Hakuna mchezo tena, sasa ni muda wetu,” alisema Saka.
Nyota huyo alisema kutwaa ubingwa huo baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika Uwanja wa Selhurst Park ilikuwa kama ndoto iliyotimia kwa wachezaji wa Arsenal.
Kiungo Declan Rice naye alisema maneno ya kuwapa moyo wachezaji baada ya kupoteza dhidi ya Manchester City yalisaidia kuibadilisha Arsenal, huku kikosi cha Mikel Arteta kikishinda mechi zote zilizobaki na kutwaa ubingwa huo kwa tofauti ya pointi saba dhidi ya City ya Pep Guardiola.


