Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, amesema ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Cape Verde baada ya muda wa nyongeza umeonyesha kuwa hakuna mchezo rahisi katika hatua za mtoano za michuano ya Dunia. Argentina ililazimika kupambana hadi dakika za mwisho baada ya Cape Verde kusawazisha mabao mara mbili kabla ya mabingwa hao watetezi kufuzu hatua ya 16 bora.
“Huu ni ujumbe kwa wale waliodai tulipata ratiba nyepesi. Tulistahili kushinda na kufuzu, lakini ulikuwa mchezo mgumu sana,” alisema Scaloni baada ya mchezo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Scaloni alisema wachezaji wake walimaliza mchezo wakiwa wamechoka sana kutokana na dakika nyingi walizocheza, huku baadhi yao wakikumbwa na maumivu ya misuli. Hata hivyo, aliwasifu kwa kupambana kwa moyo na kuonyesha tabia ya mabingwa licha ya changamoto walizokutana nazo. “Wachezaji wamechoka sana kutokana na muda wa nyongeza na wengine walipata maumivu ya misuli. Bado kuna maeneo ya kuboresha, lakini wameonyesha uthabiti mkubwa. Wanapocheza kwa moyo wanaweza kushinda changamoto yoyote,” alisema.
Kocha huyo alikiri kuwa alihofia baada ya Cape Verde kusawazisha mara ya pili kupitia bao zuri la beki wa kushoto Sidny Lopes Cabral, lakini alisisitiza kuwa hakuwahi kudharau wapinzani wao licha ya wengi kuamini mchezo ungekuwa rahisi kwa Argentina. “Nilitaka tu mchezo umalizike. Bao walilofunga lilikuwa la kiwango cha juu. Watu wengi walidhani ungekuwa mchezo mwepesi, lakini sisi tulijua usingekuwa hivyo,” alieleza Scaloni.
Akizungumzia maana ya ushindi huo, Scaloni alisema mateso na mapambano ni sehemu ya utamaduni wa soka la Argentina, akisisitiza kuwa timu yake imeimarika zaidi baada ya mtihani huo na itaendelea kupigania kutetea taji lao la Dunia. “Kuwa Muargentina ni kujua kuvumilia mateso. Cape Verde walitoa kila walichokuwa nacho, lakini tumeonyesha thamani ya jezi hii na tutaendelea kusonga mbele tukiwa na nguvu zaidi,” alisema Scaloni.


