Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, amesema anatamani kikosi chake kikumbukwe kama timu ambayo haikati tamaa kamwe, wanapojiandaa kuvaana na Uswisi katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Dunia 2026 utakaochezwa leo. Mabingwa hao watetezi wamefika hatua hiyo wakiwa hawajapoteza mechi 11 mfululizo za mashindano ya Dunia, lakini walilazimika kupambana kwa nguvu dhidi ya Cape Verde na Misri katika hatua za mtoano.
Scaloni amesema kuishabikia Argentina ni suala la mapenzi na uzalendo, akisisitiza kuwa urithi anaoutaka kuuacha ni wa timu inayopambana hadi mwisho. “Ningependa timu hii ya taifa ikumbukwe kama timu ambayo haikuwahi kukata tamaa. Tunacheza kwa ajili ya watu wetu, si kwa ajili ya ushindi pekee. Niliguswa sana nilipomwona mtoto wa miaka 10 akionyesha mapenzi makubwa kwa Argentina, hilo ndilo urithi ninaotamani kuuacha,” alisema kocha huyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo pia alimpongeza nahodha Lionel Messi, ambaye atarejea kwenye Uwanja wa Arrowhead, mahali alipofunga mabao matatu dhidi ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa Argentina kwenye michuano hiyo. Messi ana mabao nane, sawa na Kylian Mbappe katika mbio za Kiatu cha Dhahabu, huku akiwa kinara wa mabao mengi zaidi katika historia ya michuano Dunia akiwa na jumla ya mabao 21.
“Akiwa na miaka 39, baadhi ya watu wanaweza kudhani hawezi tena kufanya makubwa, lakini kwa kadri atakavyotaka kuendelea kucheza, ataendelea kuwa bora zaidi duniani. Tunachokiona mazoezini ni cha kipekee, na ni vigumu hata kufikiria alikuwa katika kiwango gani alipokuwa na miaka 23 chini ya Pep Guardiola Barcelona,” aliongeza Scaloni.
Akizungumzia mpinzani wao, Scaloni alisema Uswisi ni timu yenye uzoefu mkubwa na haitakuwa rahisi kuifunga, hasa ikiwa chini ya nahodha Granit Xhaka. “Uswisi ina historia kubwa kwenye Kombe la Dunia, ina wachezaji wenye nguvu na uzoefu mkubwa. Tunawaheshimu sana kwa sababu wameiondoa Colombia, ambayo ilikuwa ikifanya vizuri kwenye mashindano haya. Tunajua tutakuwa na mchezo mgumu, lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho,” alisema. Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya England na Norway katika hatua ya nusu fainali.


