Real Madrid wanapata penati nyingi sababu wana shambulia sana hii ni kwa mujibu wa kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone.

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu na mlinzi wa Barcelona Gerard Pique wamesema kwamba Madrid wamekuwa wakibebwa na maamuzi ya marefa kwa kupewa penati nyingi.

Zinedine Zidane alisema amechoka kusikia maneno kama hayo baada ya kuwafunga Athletic Bilbao 1-0 siku ya Jumapili, ikiwa ni mchezo wa pili mfululizo kushinda kwa penati baada ya maamuzi ya VAR baada ya Dan Garcia kumchezea madhambi Marcelo.

Madrid wamepata penati tisa katika ligi ya LaLiga kwa msimu huu wakati Athletic na Mallorca wakiwa wamepata penati kumi kila mmoja na Simeone anadhani ni kawaida kama timu itacheza vizuri katika mazingira kama hayo ili kupata maamuzi kama hayo.

“VAR inaonesha kila kitu, kabla tulikuwa hatuna uwezo wa kuona vitu ambavyo sasa tunaona. Waamuzi ni binadamu kama sisi kuna wakati wanakosea lakini kwenye VAR kila kitu kipo wazi.Alisema kwenye mkutano na wanahabari.

“Ni sawa kama wakikupa penati ni sababu upo katika nafasi ya kushambulia katika eneo la penati, kama wanavyo fanya Real Madrid.

“Maamuzi ya VAR yanaweza kukuuumiza au kukusaidia sasa ipo wazi kama ni offside, kama ni penati VAR inatujuza.

Atletico watakabiliana na Celta Vigo siku ya Jumanne lakini watamkosa nyota wao Joao Felix kufuatia kuwa na majeraha kwenye kifundo cha mguu.

Joao Felix amefunga magoli nane na kutoa asisti tatu katika michezo 34 katika mashindano yote tangu ajiunge na Atletico akitokea Benifica kwa kitita cha  €126m.

54 MAONI

  1. Diego Simeone amekuwa na mtizamo chanya katika hili na hivyo ndivyo public figure unatakiwa kuwa#meridianbettz

  2. Diego simeone yuko sahihi kabisa na kutupilia mbali kauli za rais wa Barcelona na beki wake gerrad pique kua Madrid wana bebwa Madrid n desturi yao kushambulia sana wanajua kivyovyote ile lazima beki za timu pinzan zitajichanganya kufanya makosa.ambayo yatawapa faida flan

  3. Semione yuko sahihi Madrid kwa sasa kila mechi kwao ni fainali kikubwa wanachokihitaji ni ubingwa wa laliga.

  4. Mawazo yake mbona kama sio mwanasoka? penalti inasababu ya kupatikana ,sio wachezaji kushambulia sana . Sema Meridian mnajua kutuhabarisha !

  5. Safi sana Simeon maana uwezi pata penart ukiwa haupo sehemu husika.. kwaiyo hao wanao lahumu wafanye Kama Simeon alivyosema kwamba washambulie.

  6. Ni sawa kama wakikupa penati ni sababu upo katika nafasi ya kushambulia katika eneo la penati, kama wanavyo fanya Real Madrid.

  7. Me sijaona lefa alipo kosea kwa maana lefa si hanasheria zake na jinsi nwenyewe alaivyo somea ufanyaji wake wa kazi. wajipange tu nawao washambulie kama Real Madrid na wao wapewe penati wasianze maneno maneno

  8. Real Madrid walijipanga vilivyo ni haki yaokupata penalty kama wachezaji wezao hawatakuwa makuni na ushambuliaji wao

  9. Kweli kabisah hanachoongea Diego Simeone hajaongopa amesema kweli kutokan na real Madrid alivyowaona ushambuliaji wao

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa