Serena Williams , mcheza tenisi maarufu wa Marekani, na ni binti wa Richard Williams pamoja na Oracene Price vilevile ni mdogo wa mchezaji mwingine maarufu wa tenisi Venus Williams. Alizaliwa tarehe 26 Septemba 1981 huko Saginaw Michigan.

 

Serena na Mafanikio Yake

Yeye ndiye mtoto wa mwisho kati ya mabinti watano wa Richard; Yetunde, Isha, Lyndrea na Venus. Dada yake mkubwa aliuawa mwishoni mwa 2003 huko Los Angles California, ingawa alizaliwa huko Saginawa Michigan na alilelewa Los Angles.

Familia yake ilihamia Palm Beach, Florida wakati Williams akiwa na miaka 9 tuu ili aweze kuhudhuria chuo cha tenisi cha Rick Macci.  Serena na dada yake mkubwa walisomeshwa nyumbani na baba yao kuanzia shule ya msingi hadi sekondari ili waweze kupata muda zaidi wa kufanya mazoezi ya tenisi.

Mwaka 2000 hadi 2003 alihudhuria shule ya mitindo katika taasisi ya sanaa ya Fort Lauderdale, Lakini hiyo haikumaanisha kuwa hakuwa akifuata mapenzi yake ya kucheza tenisi, na baadae alizindua safu ya mavazi ya jioni baada ya kuhitimu shule ya mitindo.

 

Serena na Mafanikio Yake

Msimamo wake katika utengenezaji wa mitindo haukufaulu na ulikatika kwa haraka, na hatimaye tenisi ilichukua nafasi ya kwanza wakati huu, na Serena alirudi kwenye viwaja vya tenisi na kushinda mataji mfululizo.

Katika kipindi hicho Serena alianzisha familia pamoja na Alexis Ohanian, mwanzilishi mwenza wa Reddit. Wenza hao walifunga ndoa na walibarikiwa mtoto katika mwaka wa 2017.  Mnamo mwaka 1999 akiwa na umri mdogo wa miaka 17, Serena alishinda U.S Open na huu ukawa ndio mwanzo wa hadhi yake kama nyota mkuu wa tenisi. Serena amecheza fainali za Grand Slams 33 na ametwaa mataji 23.

 

Serena na Mafanikio Yake

Na katika mahojiano nyota huyo maarufu wa tenisi aliwaambia waandishi wa habari kwamba haamini kusherehekea siku ya kuzaliwa kwasababu yeye ni shahidi wa Yehova na sherehe hizo hazimpendezi Mungu. Mchezaji huyo alikuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wanalipwa pesa nyingi zaidi Duniani, licha ya utajiri na umaarufu wake anajulikana sana kwa kuwa na moyo wa kutoa kwenye mashirika mabalimbali. Pia alikuwa mwanzilishi mwenza wa shule ya Sekondari ya Serena Williams nchini Kenya iliyofunguliwa Novemba 2008, Vilevile aliweza kujenga shule nchini Jamaica.

Kufikia kipindi cha mwaka 2005, Serena alitajwa kuwa mwanaspoti bora wa mwaka, na aliendelea kubaki kuwa nyota mkuu wa tenisi baada ya Grand Slam yake ya kwanza ambayo ilimpa mafanikio binafsi na kumfanya aanzishe The Serena Williams Foundation.

 

Serena na Mafanikio Yake

Ingawa wote, yeye pamoja na dada yake Venus wanajulikana sana katika undugu wa tenisi, yeye ndiye kiongozi kulingana na idadi ya mataji aliyoshinda. Venus ameshinda mataji 49, huku Serena akishinda 79.

Mchezaji huyo alikiri kuwa  Pizza ni mojawapo ya vyakula alivyovipenda sana, lakini toka awe mlaji wa mboga mboga sasa anakula pizza ya mboga mboga . Vilevile licha ya kuwa na ratiba yenye shughuli nyingi hutazama kipindi cha television ambacho hakihusiani na chochote na pia hutegemea urafiki wa binti yake kwaajili ya kusafisha akili yake.

Pia Serena ukiiacha hekaheka zake za uwanjani aliwahi kujaribu kuigiza baadhi ya filamu ambazo ni Hair Show Agent ya mwaka 2004, Days in Hell 2015, Ocean’s Eight 2018, na Pixels 2015.

 

Serena na Mafanikio Yake

 

 

 

 

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa