Simba wanatarajiwa kurejea leo kutokea nchini Malawi walipokuepo kucheza mcheza mchezo wa hatua ya awali wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Nyassa big bullets ya nchini humo.

Baada ya wababe hao wa soka nchini Tanzania kupata matokeo ugenini kwa jumla magoli mawili kwa bila wamepanga kurejea leo ambapo wanatarajiwa kufika leo mida ya saa mbili usiku.

simbaBaada ya kufika nchini wachezaji wa klabu hiyo watapewa nafasi ya kupumzika mpaka kesho ambapo watatakiwa kufika mazoezini kwajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tnazania bara ambapo watacheza na klabu ya Tanzania prisons ya mkoani Mbeya.

Klabu ya Simba itaanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya siku ya jumanne kwani siku ya jumatano watakua na mchezo huo wa ligi kuu dhidi ya Prisons.

Baada ya mchezo huo timu hiyo itakua inarudi Dar-es-salaam kujiandaa na mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Nyassa big bullets utakaopigwa siku ya jumapili tarehe 17 katika dimba la Benjamin William Mkapa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa