Simba Kushusha Vifaa Vitatu

LICHA ya kushusha vifaa mbalimbali lakini Uongozi wa klabu ya Simba umefunguka kuwa umebaki utambulisho wa wachezaji watatu ambao watafunga kazi katika dirisha hili la usajili.
Kikosi cha Simba cha awamu ya kwanza tayari kimewasili nchini Misri kwenye mji wa Ismailia kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao.
Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa “Wiki tatu tutakuwa huku kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na tumeanza mapema kutokana na watu wapya tulionao kwenye kikosi pamoja na benchi la ufundi ambapo wengi wameingia.
“Mkataba wa Kagere umebakia mwaka mmoja na hatuwezi kwenda na mchezaji ambaye hatuna mpango nae kwenye maandalizi ya msimu ujao hivyo wote wanaoenda wapo kwenye mipango yetu.
“Ndio kwanza tumeanza kushusha vifaa hii ni ishara ya kuvutia kwa ligi yetu na klabu yenyewe, na tutashusha balaa linguine hivi karibuni na tumebakiwa na saini tatu za kibabe.”

Acha ujumbe