Simba, Pamba Kuzisaka Alama Tatu CCM Kirumba Kesho

Kocha wa klabu ya Simba Sc, Steve Barker amesema mara zote mchezo dhidi ya Pamba Jiji haujawai kuwa mwepesi lakini wanaamini wanaenda kupata matokeo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu.

Simba, Pamba Kuzisaka Alama Tatu CCM Kirumba KeshoAkizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake wa Simba Sc, Morice Abraham amesema wamejiandaa vizuri kuelekea katika mchezo huo huku malengo yao makubwa ikiwa ni kuondoka na alama tatu katika uwanja wa CCM Kirumba.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Na kwaupande wa Kocha Mkuu wa Pamba Jiji, Francis Baraza, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo dhidi ya Simba SC utakaochezwa kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jjini Mwanza, huku akisisitiza kuwa wapinzani wao wanapaswa kuja kwa heshima kutokana na ukubwa na historia ya timu hiyo.

Simba, Pamba Kuzisaka Alama Tatu CCM Kirumba KeshoAkizungumza leo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo namba 85, Kocha Baraza amesema amewaelekeza wachezaji wake kupunguza makosa wanapokuwa uwanjani ili kuhakikisha wanacheza kwa umakini mkubwa na kupata matokeo chanya.

“Vijana wangu nawaambia wapunguze makosa, wakipunguza mchezo utakuwa mzuri, tusicheze na uoga wowote, tucheze kama wakubwa kwa sababu pia Pamba ni timu kubwa na ina historia yake kwahiyo mtu akija Mwanza lazima aje na heshima,” amesema Baraza.

Aidha kwa upande wa Mchezaji wa Pamba Jiji Michael Samamba amesema wanaimani kubwa ya kwenda kupata pointi 3 mbele ya Simba siku ya Kesho katika uwanja wao wa nyumbani.

Mchezo wa Simba na Pamba Jiji unachezwa kesho March 19 katika uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 10 jion.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.