UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa umempa mkataba wa muda kocha Juma Mgunda na hatma yake ipo kwa kocha mpya ambaye atakuja kukinoa kikosi hicho hivi karibuni.

Mgunda amekabidhiwa timu na mabosi wa Mashetani Wekundu baada ya kutangaza kuachana na Mserbia, Zoran Maki ambaye alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na alishinda zote.

Maki ametangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Ittihad baada ya kukiongoza kikosi hicho kushinda mbele ya Kagera Sugar na Geita Gold ila alipoteza mchezo wa Ngao ya Jamii kwa kutunguliwa mabao 2-1,Uwanja wa Mkapa.

Tayari Mgunda amekiongoza kikosi kwenye mechi mbili moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa dhidi ya Big Bullets kwenye hatua ya awali na Simba ilishinda mabao 2-0 kisha mchezo wa pili wa ligi Tanzania Prisons 0-1 Simba.

Kocha Mgunda
Juma Mgunda

Kuhusu suala la kocha mpya, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema kuwa kwa sasa kocha wa Simba ni Mgunda mpaka utaratibu utakapokamilika.

“Ipo wazi kabisa taarifa yetu kuhusu kocha mpya wa Simba ni kwamba Juma Mgunda amepewa mkataba wa kuwa kocha wa muda na hilo analifanya na matokeo yanaonekana kukiwa na taarifa nyingine tutazungumza,” .

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa