Simba Wanamtaka Kipa Mnigeria

JEFFERSON sIMBA

INAELEZWA mabosi wa Simba wamefikia muafaka wa kuvunja mkataba wa kipa wao mpya, Mbrazil, Jefferson Luis kufuatia kufeli vipimo vya afya alivyofanyiwa nchini Uturuki licha ya kuwa tayari alishajiunga na timu hiyo hali iliyowafanya kuanza kusaka mbadala wake katika mataifa ya Ulaya na Nigeria. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

 

 

Julai 23, mwaka huu Simba ilitangaza kumsajili kipa huyo kutoka Resende ya kwao Brazil kwa lengo la kuziba pengo la kipa namba moja wa timu hiyo Aishi Manula ambaye anauguza jeraha la bega ambalo alifanyiwa upasuaji.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo ambao suala la kipa huyo limekuwa likifanywa kwa usiri kuwa hatokuwa mmoja kati ya wachezaji wa timu hiyo inayotarajia kuingia nchini leo Jumatatu kutoka Uturuki baada ya kuvunja mkataba wake kufuatia kufeli vipimo vya afya alivyofanyiwa nchini humo.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Taarifa hizo zimeenda mbali zaidi baada ya viongozi wa timu hiyo kuwa tayari wameshawasiliana kocha mkuu wa timu hiyo, Robert Oliveira ‘Robertinho’ kwa kumpa majina ya makipa kutoka katika mataifa manne likiwemo Taifa la Slovenia inayopatikana barani Ulaya na Nigeria ambako anatajwa kipa wa Enyimba, John Noble anaweza kutua Msimbazi fasta kabla usajili kufungwa leo Jumatatu usiku.

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

“Jefferson hana uhakika wa kurudi kwa sababu amefeli vipimo vya afya na uongozi kwa sasa unapambana kumpata mbadala wake ili kuweza kwenda sawa kabla ya usajili kufungwa, unajua kilichopelekea hadi wamkate ni majeraha ya mara kwa mara na vipimo vimeonyesha ndiyo maana viongozi wanapambana kupata mbadala wake kwa haraka.

“Ni jambo ambalo uongozi umeamua kulifanya siri kwa sababu tayari Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Gain’ ameshaondoka na uelekeo wake ni katika mataifa ya Ulaya kwa sababu wana mataifa manne na kocha ameshapewa majina hivyo wanataka kuwahi kabla ya usajili kufungwa,” alisema mtoa taarifa.

Noble mzaliwa wa Nigeria, kwa sasa ana miaka 30, alijiunga na Enyimba mwaka 2020 ana urefu wa mita 1.92 na thamani yake ni euro 100,000 hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarkt.

Lakini kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo, Robertinho alipotafutwa na Championi Jumatatu hakutaka kuweka wazi juu ya suala hilo zaidi ya kuongelea kambi ya timu yake ilivyokuwa nchini Uturuki.

“Tumefanya kazi mambo mengi katika kipindi hichi , ikiwemo utimamu wa miili, umoja, ushirikiano, mbinu na mifumo tutakayoitumia mara kwa mara katika mechi zetu za ndani na kimataifa, kwa wachezaji kuonekana kuelewa kwa haraka zaidi, hayo mengine siwezi chochote” alisema Robertinho.

Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

Acha ujumbe